Thursday 29 September 2016

Theo Walcott aweka rekodi Ligi ya Mabingwa Uefa


Theo Walcott aweka rekodi Ligi ya Mabingwa Uefa
Walcott amefunga magoli mawili kwa mara ya kwanza katika mechi moja ya UEFA tangu Oktoba 2007 alipofanya hivyo dhidi ya Slavia Prague

Magoli mawili ya winga wa Arsenal Theo Walcott kwenye mchezo wa Kundi A michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya UEFA dhidi Basel yamemfanya atengeneze rekodi yake kwenye michuano hiyo mikubwa barani Ulaya kwa ngazi ya klabu.
Nyota huyo wa Uingereza amefunga goli lake la kichwa kwa mara ya kwanza katika michuano ya hiyo ya Ulaya.
Walcott amefunga magoli mawili kwa mara ya kwanza katika mechi moja ya UEFA tangu Oktoba 2007 alipofanya hivyo dhidi ya Slavia Prague.
Matokeo hayo yamewafanya vijana wa Wenger kucheza mechi nane bila kupoteza kwenye mashindano yote tangu walipochezea kipigo mbele ya Liverpool siku ya ufunguzi wa ligi Kuu ya Uingereza.
Ushindi wa Arsenal dhidi ya Basel ni ushindi wa kwanza msimu huu kwenye michuano hiyo baada ya kutoka sare katika mchezo wao wa kwanza dhidi ya PSG.

0 comments:

Post a Comment