Friday 10 February 2017

Simba yatangaza mchakato wa mrithi wa Mwanjale

http://michezoplus.com/wp-content/uploads/2017/02/mwanjale.png

Klabu ya Simba imetangaza kuanza kwa mchakato wa kumpata mchezaji bora wa mwezi January kwa klabu hiyo, mchakato ambao utawahusisha mashabiki wa klabu hiyo ambao watakuwa wakipendekeza majina ya wachezaji hao kupitia ukurasa wa Facebook wa klabu hiyo (Inbox).
Kwa mwezi Januari klabu ya SImba imecheza jumla ya michezo saba ambapo miwili kati ya hiyo ni kwenye ligi kuu ya VPL na Mitano kwenye kombe la Mapinduzi.

Katika michezo hiyo ya ligi kuu Simba ilicheza dhidi ya Mtibwa Sugar January 18 ambapo iliambulia sare ya 0-0 kwenye uwanja wa Jamhuri kabla ya kufungwa bao 1-0 na Azam FC January 28.
Katika Michuano ya Kombe la Mapinduzi Simba ilicheza dhidi ya KVC na kuibuka na ushindi wa bao 1-0, wakatoka ya sare ya bila kufungana, wakamfunga Jang’ombe mabao 2-0 kabla ya kumfunga Yanga kwa mikwaju ya panati 4-2 huku wakipoteza mchezo wa fainali dhidi ya Azam kwa bao 1-0.
Kwa mwezi wa Desemba, Method Mwanjali ndie alikuwa mchezaji bora wa klabu hiyo.

0 comments:

Post a Comment