Saturday 11 February 2017

Sababu tatu zitakazofanya Liverpool kufungwa na Tottenham













Sababu tatu Liverpool watafungwa na Tottenham Liverpool itasitisha wendawazimu wake wikiendi hii? Au Tottenham wataibuka washindi katika uwanja wa Anfield?

Liverpool bado hawajafanikiwa kushinda mechi ya Ligi Kuu Uingereza 2017 na wana dalili ya kukumbwa na bahati mbaya kuchezea kichapo dhidi ya Tottenham Jumamosi.
Liverpool wataikaribisha Spurs Jumamosi, mechi kubwa kuliko zote wikiendi hii Ligi Kuu Uingereza timu zote zikiwa hazitaki kupoteza pointi katika mbio za kuwania kubaki ndani ya nne bora.
Pamoja na yota Tottenham wameshinda mechi moja tu kati ya 19 za mwisho walizocheza Anfield, mechi ya mwisho walifungwa 2-1 na Liverpool kwenye Kombe la EFL mwezo Oktoba, lakini Reds bado hawajafanikiwa kushinda mechi yoyote mwaka 2017, Spurs wameshinda nne katika sita (sare 2) tangu kuanza mwaka huu.
Zifuatazo ni sababu tatu kwa nini Liverpool watafungwa na Tottenham Jumamosi.

Mbinu zao za ushambuliaji zimesomwa na wapinzani kikamilifu

Hii ndiyo sababu Tottenham watashinda. Liverpool wapo nyumbani, wapo kwenye kiwango dhaifu na presha kutoka kwa mashabiki itakuwa juu ya Klopp na kikosi chake kupata matokeo mazuri dhidi ya timu ngumu iliyo ndani ya nne bora.
James Milner Liverpool vs Tottenham
Inamaanisha watashambulia kwa wingi, lakini Spurs wapo thabiti wanapokabiliana na timu yenye kasi na safu ya beki ya Klopp italazimika kucheza kulingana na mipango ya Tottenham.
Magoli yote Liverpool wanayofunga kwa mbinu za mashambulizi ya Klopp, ambazo mwenyewe amekiri kupungukiwa ubunifu, itazidi kuwaweka matatani vijogoo na huenda wakasumbuliwa sana. Hii ilidhihirika dhidi ya Hull, Liverpool walipokuwa wakitafuta goli la kusawazisha na wachezaji nane au tisa wakiwa kwenye eneo la wapinzani wao. Mpira mmoja mrefu kutoka kwa Andrea Ronacchia ulimwezesha Oumar Niasse kufunga goli maridadi na kuwaacha Reds taabani.
Dele Alli Tottenham 04012017
Ikiwa Liverpool wanataka kushinda mechi hii, watahitaji kuwa makini sana kwani Spurs ni timu imara, hasa ukizingatia uwepo wa Dele Alli unaifanya timu hiyo kuwa tishio kuliko hapo awali. Muingereza huyo ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Januari na hiyo itampa ari kubwa kuitesa Liverpool, anafunga na kutoa pasi za magoli.

Kiwango na Uthabiti

Kwa lugha nyepesi, yote yamo mikononi mwa Tottenham. Pointi kumi na moja kutoka kwenye mechi zao tano za mwisho za ligi ikilinganishwa na ushindi mmoja wa Liverpool katika mechi kumi kwenye michuano yote hii inamaanisha Spurs ni timu yenye kiwango makini kwa mbali sana dhidi ya Liverpool. Wataingia mchezoni wakiwa wanajiamini kuwa watapata pointi tatu muhimu dhidi ya Liverpool dhaifu.
Hata hivyo Spurs wanacheza katika kiwango cha kupaa na bado wapo nyuma ya Chelsea kwa pointi tisa, bado taji halipo mbali na upeo wa macho yao lakini bado wanaweza kupoteza pointi. Kiwango chao kinaweza kuwapa fursa ya kushinda katika mechi hii.

Presha kubwa

Si tu kwamba Liverpool watakuwa na presha kubwa juu yao kutoka kwa mashabiki na wao wenyewe, Tottenham watacheza kwa mashambulizi na shinikizo kubwa kwa kasi dhidi ya kila mchezaji wa Liverpool.
Nguvu kubwa inayotumiwa na Tottenham ya Mauricio Pochettino dimbani imewafanya wachezaji wake kuwa na ufanisi mkubwa wanapokuwa na mpira kwani kila mchezaji yupo tayari kucheza kwa kujihami na kukaba kuilinda timu.
HD Jurgen Klopp Mauricio Pochettino
Liverpool wamekuwa wakisita wanapokuwa na mpira, wakihaha kupenya safu ya ulinzi ya wapinzani wao. Pasi zao si thabiti baina ya mabeki wao na hapa ndipo Spurs watakapotumia madhaifu kuwanyanyasa.
Spurs wanajua kujipanga vizuri katika safu ya ulinzi. Liverpool watapunguzwa kasi kulingana na uchezaji wa Tottenham hasa ukizingatia umahiri wa Victor Wanyama anayesambaza mipira na kukaba kwa nguvu.
Kasi ya mashambulizi ya Spurs itawawezesha kupata magoli ya haraka kama kipa wa vijogoo Simon Mignolet atafanya makosa yake ya kizembe, kwani makosa ya Mbelgiji huyo mara zote ni kwenye eneo la kona.

0 comments:

Post a Comment