Saturday 11 February 2017

Hii ni Historia ya Yanga dhidi ya timu za Comorro

Yanga Sc


Smart inakuletea mechi 3 za Yanga walizowahi kucheza dhidi ya Wakomoro
Klabu ya Yanga inajiandaa na mchezo wa klabu bingwa Afrika dhidi ya Ngaya de Mbe ya Komoro, mchezo wa hatua ya awali unaotarajiwa kupingwa tarehe 12 huko Komoro

Wana Jangwani wamepania kurudia mafanikio yao ya msimu uliopita kwa kufika kwenye makundi kombe la shirikisho Afrika
Wakomoro Ngaya De Mde' unakuwa ni mchezo wa 4 kwa klabu ya Yanga kukutana na timu za huko katika hatua hii ya mwanzo kwenye klabu bingwa wengine ni AJSM, Etoile d'or Mironsty na Komorozine
Katika michezo yote hiyo Wana Jangwani wamefanikiwa kufunga magoli 31 na wao kuruhusu magoli magoli 4 pekee, hivyo mchezo wa wikendi hii unatarajiwa Yanga kuendelea kuvuna kalamu ya magoli kama huko nyuma
Goal inakuletea mechi 3 za Yanga walizowahi kucheza  dhidi ya Wakomoro
Yanga 5 vs 1 AJSM 2007
Chini ya mwalimu Micho Yanga mwaka huu katika hatua za awali walipangwa na timu kutoka Komoro, AJSM katika mchezo wa mwanzo uliopigwa hapa nchini Wana Jangwani waliibuka na ushindi wa goli 5 kwa 1, mechi hii haikuwa na marudiano kwa sababu wapinzani hawa wa Yanga kuamua kujitoa kwenye michuano hiyo hivyo Wana Yanga kupewa tiketi ya bure kuelekea hatua inayofuata
Yanga 14 vs 1 Etoile d'or Mironsty 2009
Mwaka 2009 tena Yanga waliangukia kwa Wakomoro tena klabu ya Etoile katika hatua za mwanzo kufuzu klabu bingwa Afrika, Yanga waliokuwa chini ya Mserbia Kondic waliibuka na ushindi mnono wa jumla ya magoli 14 kwa moja, katika mchezo uliochezwa Dar es salaam waliibuka na ushindi wa holi 8 kwa 1 kabla awajaenda kuwabamiza tena goli 6 mtungi nchini komoro, licha ya kuanza vizuri msimu kwenye klabu bingwa ila Wana Jangwani walikuja kuenguliwa na Al ahly ya Misri
Yanga 12 vs 2 Komorozine 2014
Mchezo huu utabakia kumbukumbu kwa winga wa klabu ya Yanga kipindi hicho Mrisho Ngassa, kwani katika michezo 2 dhidi ya Wakomoro hawa kwani alifanikiwa kufunga goli 5 katika michezo hii miwili, mchezo wa Dar es salaam mabingwa hawa wa Ligi Kuu walishinda goli 7 kwa bila kabla ya kwenda kuibuka tena na ushindi wa goli 5 kwa 2 ugenin

0 comments:

Post a Comment