Monday 14 November 2016

Hawa ndio Mastraika bora mzunguko wa kwanza

HD Amissi Tambwe
Washambuliaji waliotesa katika mzunguko wa kwanza Ligi Kuu Bara

Ligi Kuu Tanzania Bara imefika tamati kwa duru la kwanza baada ya klabu zote 16 kucheza michezo 15 ya nyumbani na ugenini 
Mzunguko huu wa kwanza umekuwa na neema hasa kwa wachezaji wazawa kuwafunika kwa kiasi chake wageni katika kila idara hasa ya ushambuliaji
Kuna washambuliaji wengi wamefanya vizuri kwenye duru hili kwa kuweza kutumia nafasi vizuri walizo pata 
Ungana na makala hii ya Goal  inayokuletea straika bora wa mzunguko wa kwanza Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya michezo 15 
Amis Tambwe - Yanga
Mfungaji bora wa msimu uliopita kwa mabao 21 Mrundi Amis Tambwe  ameuanza msimu huu vizuri na kwa kishindo amefunga magoli 7 katika mechi 15 magoli 2 nyuma ya kinara wa mabao Shiza Kichuya, Tambwe ameendelea kuthibitisha ubora wake akiwa kwenye lango la mpinzani na anapewa nafasi kubwa ya kutetea kiatu chake cha ufungaji bora kwa msimu 
Rashid Mandawa - Mtibwa
Mandawa amejiunga na Mtibwa akitokea klabu ya Mwadui msimu uliopita, amekuwa na msimu mzuri chini ya kocha Salum Mayanga  mshambuliaji huyu wa Mtibwa amefunga magoli saba sawa na Mrundi Amis Tambwe bado ana nafasi kubwa ya kuibuka kinara wa ufungaji magoli kwa msimu huu kama raundi ya pili akiwa vizuri na kupata ushirikiano na wenzake kama mzunguko huu wa kwanza
Omary Mponda- Ndanda FC
Amefanikiwa kuliziba pengo la Atupele Green aliyetimkia JKT Ruvu kwa msimu huu, Mponda tayari amefumania nyavu mara 6 katika michezo 15 aliyo cheza kwenye duru la kwanza ni mshambuliaji mwenye nguvu na uwezo mkubwa wa kupambana na walinzi pia silaha yake nyingine ni uimara wake wa kufunga kwa kutimia kichwa

0 comments:

Post a Comment