Monday 14 November 2016

"First Eleven" Wachezaji 11 waliofanya vizuri Ligi Kuu Bara duru la kwanza

Jonas Mkude - Simba

Tunakuletea kikosi cha wachezaji 11 bora waliofanya vizuri duru la kwanza kwa kuzingatia uwezo wa mchezaji, mchango wake kwenye timu na dakika alizo cheza kwa mzunguko mzima

Duru la kwanza Ligi Kuu Bara limefika tamati kwa kila klabu kucheza michezo 15 huku Mnyama Simba akiongoza Ligi kwa tofauti ya alama mbili zidi ya Yanga pia hali siyo nzuri kwa baadhi ya klabu kama JKT RuvuTotoMajimaji kwani  wana  hati hati ya kushuka daraja
Goal  inakuletea kikosi cha wachezaji 11 bora waliofanya vizuri duru la kwanza kwa kuzingatia uwezo wa mchezaji, mchango wake kwenye timu na dakika alizo cheza kwa mzunguko mzima
1. Said kipao
Mlinda mlango wa JKT Ruvu na timu ya Taifa Stars, Kipao amecheza dakika 1350 sawa na mechi 15 za Ligi kuu na kuruhusu nyavu zake kutikiswa mara 12 licha ya kutokuwa na safu nzuri ya ulinzi kwenye timu yake ila kipa huyu amekuwa bora karibu kila mechi
2. Erick Mulilo
Amefanya kazi ya kuifanya klabu ya Stand United kuwa moja ya klabu bora kwa mzunguko wa kwanza, ni mlinzi mzuri hasa kwa washambuliaji wenye kasi na ubora wa kufumania nyavu
3. Mohamed Hussein
Ndiye mlinzi bora wa kushoto kwenye Ligi Kuu bara kwa msimu huu amekuwa msaada kwenye klabu yake kwenye ulinzi pia amekuwa akizalisha magoli mengi kwa krosi zake hatari mpaka sasa ametengeneza magoli zaidi ya matano licha ya kuwa beki
4. Andrew  Vicent
Amefanikiwa kuingia kwenye kikosi cha kwanza chini ya kocha Hans Pluijm, beki huyu ameunda ngome ngumu na kufanya klabu yake kuruhusu magoli 7 pekee tangu kuanza kwa msimu
5. Method Mwanjale
Mlinzi wa kati wa klabu ya Simba na  raia wa Zimbabwe, Mwanjale licha ya kuonekana mkubwa kiumri ila amefanikiwa kucheza mechi zote 15 za Ligi Kuu pekee na kuruhusu klabu yake  kufungwa magoli sita, mkongwe huyu ameonesha nidhamu kubwa mpaka sasa

6. Jonas Mkude
Kiungo mkabaji wa Simba Mkude ndiye aliyekuwa akiilinda vizuri safu yake ya ulinzi kutopata madhara licha ya kucheza chini ila alitengeneza nafasi pia za kufunga kwa washambuliaji wake,  Mnyama ameongoza Ligi kutokana na ubora pia wa kiungo huyu mkabaji
7. Simon Msuva
Ndiye kinara wa kutengeneza magoli kwenye mzunguko wa kwanza katika mechi 15 winga huyu katoa pasi 13 za magoli na kufunga magoli 7 ikiwa ni  idadi kubwa kuliko mchezaji yeyote 
8.Kenny Ally 
Ni jina geni kwenye soka hapa nchini, kiungo huyu wa Mbeya City amefunga magoli 3 kwenye michezo 15  amefanya kazi kubwa raundi hii ya kwanza uwezo mkubwa wa kumiriki dimba la kati na kuchafua mbinu za mpinzani hali kadhalika uwezo mkubwa wa kufunga kwa magoli ya mbali
9.Rashid Mandawa
Amefunga magoli 7 mawili 2 nyuma ya kinara wa magoli, mshambuliaji wa Mtibwa amekuwa na msimu mzuri kwa mzunguko huu wa kwanza na ndiye mzawa pekee mwenye magoli mengi kwenye nafasi anayo cheza ya mshambuliaji wa kati
10. Amis tambwe
Mfungaji bora wa msimu uliopita licha ya kutocheza kwa mechi zote 15 kama wengine ila bado yupo juu kwenye chati ya ufungaji, Mrundi huyu ameendelea kuwa tishio kwa mabeki wengi hapa nchini
11. Shiza Kichuya
Ndiye mchezaji bora wa Ligi Kuu kwa mzunguko wa kwanza winga huyu amekuwa na mchango wa moja kwa moja kwenye timu yake, Kichuya ndiye kinara la magoli akiwa amefunga mara 9 na kutoa pasi 5 za magol

0 comments:

Post a Comment