Tuesday 13 September 2016

Jinsi kikosi cha Yanga kinavyompa hofu Omog

Kikosi cha Yanga champa hofu Omog

Pamoja na kikosi chake kufanya vizuri kwenye mechi za ligi ya Vodacom lakini hofu ya Omog ipo kwa mabingwa watetezi Yanga

Kocha mkuu wa Simba Joseph Omog, amesema pamoja na kikosi chake kufanya vizuri kwenye mechi za ligi ya Vodacom lakini hofu yake kubwa ipo kwa mabingwa watetezi Yanga.
Omog ameiambia Goal, Yanga imeonekana ni timu iliyojipanga vizuri na wachezaji wake wanaonyesha kuwa na uzoefu mkubwa na kucheza kwa malengo tofauti na timu nyingi.
"Naweza kusema Yanga ndiyo timu ambayo inanipa presha kutokana na ubora waliokuwa nao kwa kila mchezaji na timu nzima," amesema Omog.
Omog  huyo amesema pamoja na kwamba yeye ni kocha wa Simba lakini anaipa nafasi kubwa Yanga kuibuka mabingwa wa Ligi ya Vodacom msimu huu kama hawatofanya makosa mengi na kuzitoa nafasi timu nyingine.

0 comments:

Post a Comment