Thursday 29 September 2016

Pogba aweka rekodi yake ya pasi Europa Man United ikishinda dhidi ya Zorya

Pogba aweka rekodi yake Europa Man United ikishinda dhidi ya Zorya

Supastaa huyo wa United mwenye umri wa miaka 23 amezidi kuimarika katika kila mechi anayocheza akiwa na Mashetani Wekundu

Licha ya kiwango kisichoridhisha cha Mashetani Wekundu dhidi ya Zorya Luhansk katika mechi yao ya Ligi ya Uropa Alhamisi, takwimu mpya zinaonesha kuwa Paul Pogba alicheza katika kiwango kikubwa.
Mchezaji huyo ghali zaidi duniani alikuwa muasisi wa mlolongo wa pasi katika safu ya kiungo licha ya kutoleta madhara ndani ya eneo la hatari la wapinzani.
Marouane Fellaini alicheza eneo la kati Pogba alipocheza kama mchezaji asiye na majukumu, na takwimu zimeoneysha hasa ubora wa Mfaransa huyo.
Kwa mujibu wa kampuni ya data za soka Opta, mkali huyo alipiga pasi 107 zilizokamilika dhidi ya miamba wa Ukraine; pasi nyingi zaidi akiwa na United.

0 comments:

Post a Comment